News
Askofu Anyolo: Kadinali Njue Hatahudhuria Conclave
Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Nairobi limetangaza kwamba John Kadinali Njue, hatashiriki Kongamano la kumchagua Papa mpya wa Kanisa Katoliki duniani.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa na Kanisa hilo siku ya Jumanne, Kadinali Njue ambaye anastahili kupiga kura katika Kongamano hilo maarufu Conclave alikuwa amepokea mwaliko rasmi kutoka Shirika la kitume ili kuhudhuria Kongamano hilo ambalo linafaa kuanza rasmi tarehe 7 mwezi Mei mwaka huu lakini hataweza kusafiri.
Kanisa hilo limesema Mwakilishi wa Papa nchini Kenya Askofu Hubertus Marie Van Megen baada ya kushauriana na ofisi ya Askofu mkuu wa Nairobi Phillip Anyolo, alitoa taarifa kwamba Kadinali Njue mwenye umri wa miaka 80 hataweza kusafiri hadi Vatican- Roma kwa Kongamano hilo.
Picha kwa hisani
Askofu Anyolo amewataka waumini wa Kanisa Katoliki kuombea makadinali wanaochukua jukumu zito la kumchagua Papa mpya huku akihimiza maombi zaidi kwa ajali ya Afya na ustawi wa Kadinali Njue.