News

Wafanyikazi wa Vibarua Katika Hospitali ya Mariakani Wameanza Mgomo Baridi

Published

on

Wafanyikazi wa vibarua katika Hospitali ya Mariakani kaunti ya Kilifi wameanza mgomo baridi wakilalamikia usimamizi duni wa hospitali hiyo sawa na kukosa kulipwa mishahara yao kwa kipindi cha miezi miwili.

Wakiongozwa na Mwenyekiti wao Rajab Juma Mumo, wafanyikazi hao wa vibarua wamesema kumekuwa na sintofahamu katika ulipaji mishahara kwani licha ya wafanyikazi hao kuwa zaidi ya 70 ni wafanyikazi 40 pekee watakaopewa kandarasi na kampeni binafsi.

Mumo amelalakia kutojumuishwa kwa wafanyikazi hao katika mikataba mipya ya uajiri sawa na kutopewa mishahara yao kwa kipindi cha miezi miwili kutoka kwa usimamizi wa hospitali hiyo pamoja na serikali ya kaunti ya Kilifi.

Aidha wamesema wamefanya kazi katika Hospitali hiyo ikiwemo kusafisha mazingira miongoni mwa kazi zengine kwa zaidi ya miaka sita bila ya kupewa ajira za kudumu.

Hata hivyo juhudi za Wanahabari wetu kubaini uhalali wa madai hayo ziligonga mwamba kwani wasimamizi wa hospitali hiyo sawa na viongozi kutoka serikali ya kaunti ya Kilifi wamekataa kuzungumzia swala hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version