National News
Wanaotafuta Nafasi ya Mwenyekiti wa IEBC Kuhojiwa Jumatatu
Jopo la uteuzi wa Makamishna wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC limetangaza kuanza zoezi la kuwapigwa msasa watu 11 ambao walituma maombi ya kujaza nafasi ya Mwenyeti wa Tume ya IEBC.
Joto hilo limetoa orodha ya zoezi hilo, kwamba siku ya Jumatatu tarehe 24 mwezi huu wa Machi, watakaohojiwa ni pamoja na aliyekuwa msajili mkuu wa idara ya Mahakama nchini Anne Amadi, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya utekelezaji Katiba CIC Chalse Nyachae, Edward Katama kutoka TransNzoia na Abdulqudir Lorot kutoka Baringo.
Mwengine ni pamoja na Erastus Edung Ethekon, Francis Kakai Kissinger, Joy Brenda Masinde-Mdivo, Jacob Ngwele Muvengei, Lilian Wanjiku Manegene, Robert Akumu Asembo, na Saul Simiyu Wasilwa, ambao wataohojiwa siku ya Jumanne tarehe 25 mwezi huu.
Mwenyekiti wa jopo hilo Dkt Nelson Makanda amesema wale wanaotafuta nafasi ya makamishna watahojiwa kuanzia siku ya Jumatano tarehe 26 hadi Jumapili tarehe 30 na watu 105 wamejumuishwa katika orodha ya watakaohojiwa ili kujaza nafasa za Makamishna.
Dkt. Makanda amesema jopo hilo litafanya kila juhudi kuhakikisha wakenya wanapata makamishnaalio waadilifu na ambao wako tayari kufanya kazi bila ya kushurutishwa na mtu yeyote.
Dkt. Makanda amewarai wakenya ambao wako na dukuduku na watu walioorodheshwa kupigwa msasa kuwasilisha lalama zao kwa maandishi ili jopo hilo lichukue hatua za mapema.
“Wananchi wanaombwa kuwasilisha kwa maandishi na kiapo taarifa zozote zinazohusiana na wale walioorodhesha kuhojiwa kwa nafasi ya Mwenyekiti wa IEBC ili kuzuia kuteuliwa kwa viongozi wasio waadilifu”, Dkt Makanda.