News
WAVUVI MJINI KILIFI HAWANA VIFAA VYA KISASA VYA UVUVI
Mwenyekiti wa wa wahudumu wa maboti Kilifi mjini kaunti ya Kilifi, Shallo Issa maarufu captain Shallo amesisitiza haja ya wavuvi wa eneo hili kuimarishwa kupitia vifaa vya kisasa vya uvuvi.
Akizungumza na Coco Fm, Shallo amesema kuwa wavuvi wengi wanashindwa kwenda kuvua kwenye maji makuu kutokana na ukosefu wa boti za kisasa sawa na nyavu na mishipi ya kisasa.
Licha ya kuwa mradi wa maendeleo ya jamii, kiuchumi na uvuvi KEMFSED uliwasaidia kwa kuwapata baadhi boti, Shallo amesema bado boti hizo ni ndogo mno na haziwezi kuhimili mawimbi kwenye maji makuu jambo linalopelekea shinikizo zao za kuitaka serikali kuwaimarisha kwa vifaa Zaidi vya kisasa.
Kufuatia hilo Shallo amesema kuwa wavuvi wengi wanaendelea kuathirika kutokana na wao kushindwa kuvua samaki kwa wingi ikizingatiwa kwamba samaki wengi hupatikana kwenye maji makuu.