News
Watene: CBC itawafaidi wakenya iwapo itaangazia changamoto za wananchi.
Mgombea wadhifa wa urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2027 Robert Watene amesema mfumo wa mtaala wa elimu nchini CBC utawafaidi wakenya iwapo utaangazia changamoto wanazokumbana nazo wakenya.
Akizungumza katika mahojiano ya kipekee na Coco FM, Watene amesema nchi ya Kenya imesalia nyuma kielimu na kimaendeleo tofauti na nchi zingine kwani mfumo uliyopo nchini haujampa mtoto ujuzi wa kumasaidia kujiajiri baada ya masomo.
Akitolea mfano nchi ya Ujerumani, Watene amesema mfumo wao huangazia kuwapa wanafunzi ujuzi jambo ambalo kulingana naye limepunguza ongezeko la ukosefu wa ajira nchini humo.
“Masomo ya nje wanafocus sana na problem za kwao hata ukiangalia zile curriculum zao zinajaribu kusolve zile matatizo ambazo wako nazo unapata mtu amemaliza kusoma na tayari ako na skill ya kutengeneza magari na kadhalika” alisema Robert Watene.
Watene amesema mfumo mpya wa CBC unastahili kuwa kama vyuo vya kiufundi ili kuwasaidia vijana kujiajiri pindi tu wanapokamilisha masomo yao.
Wakati uo huo amesema iwapo atapata nafasi ya kuongoza taifa la Kenya atahakikisha anabadilisha maji ya bahari kuwa maji safi kwa matumizi ya binadamu ili kuwapunguzia dhiki wakaazi wa eneo la Pwani.
“There people who are walking kilometers and kilometers to get water ila hakuna kiongozi ambaye amesimama kuhakikisha kwamba haya maji yetu ya bahari yanageuka maji safi ya kunywa ili kupunguza magonjwa yanayosababishwa na maji chafu” alidokeza Watene.
Taarifa ya Elizabeth Mwende.