News
Wapwani Tuungane: Asema Mwanasiasa eneo la Marafa
Aliyekuwa mwakilishi wadi wa Marafa, Renson Kambi Karisa amesisitiza haja ya viongozi wa pwani kushirikiana katika kuimarisha ukanda wa pwani.
Kambi alisema kuwa kupitia mshikamano huo ndoto ya pwani kupata rais inaweza kufanikishwa kwa wepesi.
“Uhasama wa mara kwa mara baina ya viongozi wa pwani unachangia ukanda huu kudorora kimaendeleo” alisema Kambi.
Aidha Kambi aliwakashifu vikali viongozi wa pwani wanaoendekeza upinzani miongoni mwao kwa manufaa ya viongozi wa maeneo mengine, akisema kuwa swala hilo linachangia kuzorota kwa ukanda wa pwani.
Taarifa ya Hamisi Kombe