News

Wanasiasa wahimiza wakaazi kuunga mkono Serikali

Published

on

Baadhi ya viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Taita Taveta sasa wanashinikiza wakaazi wa kaunti hiyo kuunga mkono serikali ya Kenya Kwanza wakisema inaendeleza mikakati kuhakikisha inatekeleza miradi ya maendeleo katika kaunti hiyo.

Wakiongozwa na Mwakilishi wa wadi ya Chawia Joseph Mabishi alisema serikali ya Kenya Kwanza imeonyesha nia ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika kaunti hiyo na pwani kwa ujumla sawa na kutoa nafasi za kazi serikalini, hivyo kuna haja ya kuiunga mkono na kuipa muda ili ifanikishe ahadi zake kwa wananchi.

Aidha, Mabishi aliwataka viongozi wa kaunti hiyo ya Taita Taveta kuwa na agenda ya kuwahudumia wananchi badala ya kuwagawanya kupitia mirengo yao ya kisiasa.

‘’Tunataka viongozi ambao wanakuja kuleta nchi pamoja na kutujumuisha na pia kutekeleza maendeleo, sio wanasiasa wachochezi’’ Alisema Mabishi

Vilevile, Mabishi alitoa wito kwa viongozi wa kaunti ya Taita Taveta kuashirikiana ili kuiboresha kimaendeleo.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version