News
Maadhimisho ya ugonjwa wa Selimundu duniani
Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya ugonjwa wa Selimundu maarufu Sickle cell Aenemia, ukosefu wa hamasa za kutosha miongoni mwa jamii umetajwa kuchangia ongezeko la kusambaa kwa ugonjwa huo hasa maeneo ya Pwani.
Kulingana na Daktari wa watoto wenye ugonjwa wa Selimundu na pia ni mtafiti katika taasisi ya utafiti wa matibabu nchini KEMRI kaunti ya Kilifi Mejumaa Mohammed, amesema kwamba watoto wengi wanaadhirika na ugonjwa huo pasi nao kutambua kwamba wanaugua Selimundu.
Daktari Mejumaa alibainisha kwamba baadhi ya dalili za ugonjwa huo kwa watoto huonekana miezi minne hadi sita baada ya mtoto kuzaliwa.
“Ni jukumu la wazazi kuwa makini na afya ya watoto wao kwani magonjwa mbalimbali ya kuchipuka na kuathiri afya ya mtoto hasa Selimundu huonekana baada ya miezi mine hadi sita na kwamba ni hatari kwa afya ya mtoto kama hutabainika kwa haraka”, alisema Mejumaa.
Msimamizi wa wagonjwa wa magonjwa yasioambukizwa John Mosi, alisema Kilifi ni baadhi ya maeneo yaliothirika pakubwa na ugonjwa huo huku akisema kwamba wazazi walio na chembechembe za ugonjwa wa Selimundu wanapooana huenda wakapata mtoto aliyeadhirika na ugonjwa huo.
Taarifa ya Elizabeth Mwende