Sports
Wakenya Kuzindua Uhasama Mbio Za Oregon Prefontaine Classic
Wanariadha nguli wa Kenya watatumia mbio za makala ya Oregon Prefontaine Classic kama mbio za majaribio kabila ya mbio za Dunia mjini Tokyo Japan badaye mwakani.
Bingwa wa Olimpiki mbio za mitaa 5000 na 10,000 Batrice Chebet anatarajiwa kuongoza wenzake katika mbio hizo wikendi hii ambapo chama cha riadha AK inatarajiwa kukiteuwa kikosi chake cha dunia.
Wanariadha wengine ambao wanarajiwa kutimka mbio hizo mjini Oregon Marekani ni pamoja na ;bingwa wa mbio za kilomita 10 Agnes Ngetich,bingwa wa zamani mbio za mitaa 10000 Caroline Nyaga,wengine ni pamoja na: Margaret Akidor, Maurine Jepkoech, Janeth Chepngetich, Sarah Wanjiru, Caroline Kariba, na Hellen Ekalale.
Sheria za chama Raidha nchini AK zinaarifu kwamba washindi watakaomaliza nafasi za kwanza na ya pili wanafuzu moja kwa moja katika mashindano ya Dunia.