News
Wakaazi Wahimizwa kutembelea Hospitali ya Malindi kwa Ukaguzi wa Kiafya
Daktari mkuu anayesimamia kitengo cha masuala yanayohusu kifua katika hospitali kuu ya Malindi kaunti ya Kilifi Anderson Ngala amewahimiza wakaazi kufika hospitalini iwapo watahisi maumivu kifuani.
Daktari Anderson amesema hatua hiyo itasaidia kufanyiwa vipimo ili kubaini ikiwa wanaugua ugonjwa wa kifua kikuu au la.
Kulingana na Daktari Anderson, watu wengi wamekuwa wakipuuza kufika hospitalini licha ya kuhisi maumivu, akisema ugonjwa huo unapogundulika mapema inakuwa rahisi kutibiwa.
Daktari Anderson amewataka wakaazi kuchukua tahadhari ili kujikinga dhidi ya maambukizi ugonjwa wa kifua kikuu.
Wakati huo huo amesema kupima kikohozi ni bure huku akitaja baadhi ya dalili za ugonjwa huo wa kifua kikuu.