Business

Wafanyabiashara wa Maembe Mariakani Walia na Hasara Kufuatia Mvua

Published

on

Wafanyibiashara wa kuuza maembe katika eneo la mariakani kaunti ya kiliifi wanasema kuwa msimu huu wa mvua biashara iko chini ikilinganishwa na msimu wa kiangazi.

Kulingana na Amina Menza licha ya kuwa maembe ni mengi idadi ya wateja imepungua kutokana na baridi hali ambayo inasababisha maembe kuharibika.

Akizungumza na cocofm Menza amesema mara kwa mara wamekuwa wakikadiria hasara hasa maembe yakinyeshewa huharibika.

Aidha wameitaka serikali kujenga viwanda vya maembe hasa eneo la pwani ili kuwasaidia kuuza maembe na kuikimu kimaisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version