Business
Wafanyabiashara Kilifi Walalamikia Hasara Kutokana na Wachuuzi Barabarani
Wafanyibiashara mjini kilifi kaunti ya kilifi wanasema kuwa biashara mbalimbali zimedorora kutokana na ongezeko la idadi ya wachuuzi ambao wanachuuza kando kando mwa barabara kila mahali.
Kulingana na wafanyibiashara hao wanakadiria hasara kwani wateja wengi hawaendi sokoni ikizingatiwa kuwa wanaweza kupata bidhaa kwa urahisi kutoka kwa wachuuzi hao.
Wakizungumza na cocofm wafanyibiashara hao wanasema licha ya wao kulipa ushuru hakuna biashara zozote wanaendeleza kufuatia idadi ndogo ya wateja.
Aidha wametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Kilifi kudhibiti wachuuzi hao.