Business

Wachuuzi wa njugu mjini Kilifi waongezeka.

Published

on

Idadi ya wachuuzi wa njugu mjini Kilifi kaunti ya Kilifi imetajwa kuongezeka msimu huu ikilinganishwa na hapo awali.

Kulingana na Kazungu Kaingu, vijana wengi punde wanapomaliza shule huingilia biashara hiyo hali ambayo imepelekea wanaofanya biashara hiyo kuongezeka kwa wingi.

Akizungumza na coco fm Kazungu alisema kuwa ongezeko la idadi ya wafanyibiashara hao imechangia mauzo ya bidhaa hiyo kudorora kwani idadi ya wateja pia imepungua.

Hata hivyo Kazungu alisema kuwa bei ya njugu imepanda kwani kwa sasa wananunua kilo moja kwa shilingi mia tatu tofauti na awali ambapo walikuwa wakinunu kwa shilingi mia moja na hamusini.

Aidha gharama ya maisha ilitajwa kuchangia kudorora kwa biashara hiyo huku serikali ikitakiwa kuweka mikakati ya kupunguza gharama ya maisha ili wananchi waweze kuimarika kiuchumi.

Taarifa ya Pauline Mwango

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version