Business
Utalii waimarika Watamu kaunti ya Kilifi
Wadau wa sekta ya utalii wadi ya Watamu kaunti ya Kilifi wameripoti kuimarika kwa sekta ya utalii eneo hilo mwaka wa 2025 ikilinganishwa na mwaka uliopita wa 2024.
Wakiongozwa na mkurugenzi wa hoteli ya Seven Island Ravi Rora, wadau hao walisema kwa sasa sekta hiyo imesajili jumla ya asilimia 25 ya watalii wanaozuru eneo hilo, huku wengine wakitarajiwa kutembelea eneo hilo siku zijazo.
Rora aidha alifichua kuwa asilimia kubwa ya hoteli za Watamu tayari zimepokea idadi kubwa ya maombi ya watalii watakaozuru eneo hilo kwa likizo ya mwezi Disemba.
Wakati huo huo mkurugenzi huyo alibainisha kuwa idadi kubwa ya watalii hao ni wa asili ya kiitaliano, Wafaransa miongoni mwa wa kutoka nchi nyingine.
Alieleza matumaini kuwa hali hiyo itaimarisha uchumi wa kaunti ya Kilifi na Kenya mzima kwa ujumla.
Taarifa ya Pauline Mwango.