Sports
United Wamewasilisha Ofa Kupata Mshambulizi Sseko
Klabu ya Manchester United imewasilisha rasmi ofa kwa klabu ya RB Leipzig kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Benjamin Šeško.
Ofa hiyo inakadiriwa kufikia jumla ya Euro Milioni 85 (€85M) ambapo €75 milioni ni malipo ya moja kwa moja, huku €10 milioni yakiwa ni nyongeza inayotegemea mafanikio ya mchezaji huyo.
United wanaamini kuwa Šeško, mwenye umri wa miaka 22, ana nia ya kujiunga na kikosi cha Old Trafford. Hata hivyo, hadi sasa RB Leipzig bado hawajatoa majibu rasmi kuhusu ofa hiyo.
Kwa upande mwingine, Newcastle United pia wanaendelea na juhudi za kumshawishi mchezaji huyo ajiunge nao.