Rais Ruto aonyo wanasiasa dhidi ya vurugu Makanisani

Rais Ruto aonyo wanasiasa dhidi ya vurugu Makanisani

Rais William Ruto amewaagiza maafisa wa usalama kuhakikisha maeneo ya makanisa na sehemu zengine ya kuabudu zinapewa ulinzi wa hali juu ili kuhakikisha waumini wanashiriki ibada zao kwa amani.

Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa la PEFA kaunti ya Nairobi, Rais Ruto aliema ni lazima mazingira ya nyumba za ibada yalindwe dhidi ya vurugu za kisiasa, akisema tabia hizo zinafaa kukoma.

Kiongozi wa nchi, aliwahimiza wanasiasa kujitenga na siasa za vurugu kwenye nyumba za ibada, akiwataka kutafuta uongozi na siasa zao nje ya mazingira ya makanisa kwani maeneo hayo yanafaa kupewa heshima.

Akigusia suala la kisiasa, Rais Ruto alionekana kujipigia debe kisiasa ili kudhibiti kiti chake katika uchaguzi mkuu ujao, akisisitiza suala la Tutam wakati wakenya wanapokaribia uchaguzi mkuu.

“Unawezapiga siasa na kutafuta uongozi kila mahali lakini maeneo ya makanisa hiyo hatutakubaliana nayo, makanisani na kwenye madhabahu ni mahali pa kuheshimiwa, kwa hivyo wanasiasa tutafute mahali kwengine kwa kuleta fujo huko haitakubaliwa na maafisa wa usalama ni lazima muweke ulinzi kwa waumini”, alisema Rais.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kitaifa wa Chama cha ODM ambaye pia ni Gavana wa Homabay Gladys Wanga alisema viongozi wa chama hicho wamempa ruhusu Kinara wao Dkt Oburu Oginga kufanya mazungumzo na vyama vyengine ili kubuni Muungano wa kisiasa.

“Sisi kama wanachama wa ODM tumemruhusu Kiongozi wetu Dkt Oburu Oginga kufanya mazungumzo na vyema vingine vya kisiasa vilivyo na ajenda na kusongeza Kenya wetu mbele”, alisema Wanga.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi