Sports

Uganda Cranes Kileleni Kundi C Michuano Ya CHAN

Published

on

Timu ya taifa ya Uganda, maarufu kama Uganda Cranes, imekwea kileleni mwa Kundi C baada ya ushindi wa mabao 2–1 dhidi ya Niger jana kwenye uwanja wa Nelson Mandela, mjini Kampala.

Mshambulizi nyota na nahodha Allan Okello aliwaweka Uganda Cranes kifua mbele dakika ya 21, dakika chache baada ya kupoteza nafasi ya penalti, kabla ya mshambulizi Joel Sserunjji kuongeza bao la pili dakika ya 56 kipindi cha pili.

Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa wenyeji wenza wa CHAN, baada ya kuanza kwa kusuasua walipopoteza mechi ya ufunguzi kwa mabao 3–0 dhidi ya Algeria, maarufu kama The Desert Foxes.

Uganda sasa ina alama 6 baada ya michezo mitatu, ikifuatiwa na Algeria yenye alama 4, Afrika Kusini ikiwa nafasi ya tatu pia na alama 4, Guinea ikishika nafasi ya nne na alama 3, huku Niger ikiburuza mkia bila pointi yoyote kwenye michezo ya kundi hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version