National News
Tungule: Tatizo Kubwa la Ganze ni Umaskini
Mbunge wa Ganze Kenneth Kazungu Tungule amesema tatizo kubwa ambalo linakumba eneo bunge hilo ni umasikini.
Akizungumza kwenye kipindi cha Coco Asubuhi, Tungule amesema eneo bunge hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maji, umaskini, ukosefu wa ajira kwa vijana miongoni mwa maswala mengine.
Kulingana na Tungule, hali hiyo imechangiwa na ukosefu wa vitega uchumi ambavyo vinaweza kutegemewa na wenyeji ili kujikimu maisha.
“Tuko na changamoto nyingi sana Ganze ambazo zinafaa kutatuliwa kwa wakati lakini tatizo kubwa zaidi ni kwamba hatuna vitego uchumi ambavyo vinaweza kubadili uchumi wa maeneo hayo ndio maana wengi wa wakaazi wanategemea uchomaji makaa na hali hii imechangia eneo la Ganze kuwa jangwa”, Tungule.
Wakati huo huo amesema anaendeleza mikakati mbalimbali kukabiliana na changamoto za eneo bunge hilo huku akiwahimiza washikadau mbalimbali kuunga mkono swala la uwekezaji katika eneo bunge hilo.