News
Timamy: Tulinde Raslimali ya Umma
Gavana wa Lamu Issah Timamy amewataka wakaazi wa kaunti ya Lamu kuzilinda raslimali zilizoko kwenye kaunti hiyo.
Akizungumza katika eneo la Mbwajumwali Gavana Timamy amesema kumekuwa na visa vya uporaji wa mali ya serikali ikiwemo majengo kukatwa milango, madirisha na hata vyuma.
Timamy amesema fedha ambazo zinatumika kujenga majengo hayo ni fedha za umma na akawataka wenyeji kuwa mstari wa mbele kuzilinda raslimali za umma.
Ameyazungumza haya baada ya kuona ukumbi wa mikutano uliojengwa na serikali ya kaunti ya Lamu kuvunjwa milango na madirisha hali ambayo itailazimu serikali ya kaunti hiyo kugharamika tena.