Sports

Taifa Stars Ya Tanzania Yapepea Mechi Ya Pili Ya CHAN

Published

on

Timu ya taifa Stars ya Tanzania imeweka guu moja kuingia kwenye hatua ya robo fainali taji la CHAN. Hii ni baada ya ushindi wa pili mfululizo safari hii wakipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mauritania uwanjani Benjamin Mkapa nchini Tanzania.
Bao hilo la kipekee lilitiwa wavuni na beki Shomari Kapombe dakika ya 89 kipindi cha pili baada ya milango kukauka kipindi cha kwanza wa mchuano huo.
Taifa Stars imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Kundi B ikifikisha pointi 6 baada ya mechi mbili.
Katika matokeo ya mechi nyingine  ni kwamba taifa la Burkina Faso ilirejesha tabasamu kwa mashabiki wake baada ya kuvuna ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya Central Afrika Republic,timu hiyo ilikua imepoteza mechi ya ufunguzi magoli 2-0 dhidi ya mwenyeji Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version