Sports

Starlets Kucheza Fainali Ya CECAFA Dhidi Tanzania

Published

on

Kikosi cha soka akina dada kushuka dimbani kucheza dhidi ya Twiga Stars Ya Tanzania kwenye fainali ya kipute cha CECAFA Afrika Mashariki ugani Azam Sports Complex.

Vipusa wa kocha Beldine Odemba wameshinda mechi zote tatu ikiwemo kuwalaza Sudan Kusini magoli 4-0 mechi ya siku ya Alhamisi huku wakiwa wamekusanya alama 9 sawa na wenyeji Tanzania kwenye mashindano ya mwaka huu.

kwa mujibu wa mwalimu huyo wanatarajia mechi ngumu dhidi ya wapinzani wao kwani wako nyumbani na timu bora pia.

“Tuko tayari kwa mechi ya mwisho ambayo pia ni fainali kila mmoja anajua tumekua vizuri katika mashindano haya ila Tanzania ni mpinzani mkubwa katika fainali ya leo kwa sababu pia hawajapoteza mechi kama sisi.”

Mechi hiyo inangoa nanga saa 12.00 jioni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version