Ujenzi wa Uwanja mpya wa Voliboli waanza Kilifi, Huku Ujenzi wa uwanja wa mpira wa vikapu ukikaribia kukamilika

Ujenzi wa Uwanja mpya wa Voliboli waanza Kilifi, Huku Ujenzi wa uwanja wa mpira wa vikapu ukikaribia kukamilika

Vijana na wapenzi wa mchezo wa Voliboli Kilifi sasa wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kilio chao cha kupata uwanja mpya kuonekana kujibiwa hivi karibuni.

Kulingana na mwanakandarasi mkuu wa ujenzi wa uwanja huo Athman Muhaji ni kwamba zaidi ya shilingi milioni 1.5 imetengwa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo mpya ikiwa ni zaidi ya laki mbili kwa fadha zilizotumika kujenga uga wa Basketiboli ugani Karisa Maitha.

“Kama huu mradi kuisha itagharimu kama shilingi milioni 1.6 ama 1.4 hivi ili kupata uwanja bora mno naamini uwanja huo utaisha kwa kipindi cha wiki mbili hivi.”

Kwa Upande wake katibu mkuu mwandalizi wa chama cha Voliboli kaunti kilifi Henry Nyambu amekaribisha kwa moyo mkunjufu hatua hiyo mpya akikiri kwa muda na miaka mingi wamecheza kwenye vumbi na kuona uwanja mpya unajengwa ni jambo la kutia moyo akimpongeza mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya.

“Kuona mweshimiwa anajenga uwanja wa kimataifa wa Voliboli hakika ni fahari lakini pia ni historia kwani hata kwa kaunti zingine na wapinzani wetu hawana viwanja vya haina hii kwa hiyo nimshukuru saana mheshimiwa kwa kazi hii kuntu,naamini itakua ni uwanja wa Ubora zaidi ya kujivunia kama wanakilifi.”

Kulingana na mshirikishi wa Sokoni Ward Johnson Charo ni kwamba huu ni mwamko mpya Kilifi kwani viwanja vya aina hii vimekua nadra mno kuzipata na sasa ni fahari ya kila kijana kutumia vipaji vyao vilivyo katika michezo hiyo.

“Kwa Muda vijana wamekua wakicheza katika viwanja vya vumbi ila sasa ni mwamko mpya kweli kweli kuendeleza kuonyesha vipaji vyao katika viwanja vyenye ubora.”

Haya yanajiri huku uwanja mpya wa mpira wa vikapu ukikamilisha katika uwanja huo uo zote kwa ufadhili wa mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya.