News

Spika Khatri, awakosoa wanasiasa kwa kutoangazia maendeleo

Published

on

Spika wa bunge la kaunti ya Mombasa Aharub Khatri amezidi kuwakosoa viongozi wa kisiasa katika kaunti hiyo kutokana na kile ambacho anadai wanaendeleza siasa ambazo hazina manufaa kwa wakaazi.

Akizungumza katika eneo bunge la Mvita, Khatri alisema inasikitisha kuona viongozi hao wanawatumia wananchi visivyo kwa manufaa yao binafsi badala ya kuwatekelezea miradi ya maendeleo.

Khatri alisema ni jukumu la viongozi ambao walichaguliwa kuhakikisha wanatekeleza miradi ya maendeleo kama walivyoahidi wakati wa kampeni zao za uchaguzi wa mwaka wa 2022.

‘’Ndani ya uongozi ukiangalia mara nyingi watu huwa hawapendi kutajirisha maskini, wanapenda watu waendelee na umaskini’’aisema Khatri

Wakati huo huo, aliwahimiza vijana katika kaunti ya Mombasa kujiepusha na viongozi ambao wanalenga kuwatumia visivyo kwa manufaa yao binafsi na kuhakikisha katika uchaguzi mkuu wa 2027 wanawachagua viongozi waadilifu.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version