News
Soma la Hisababiti ni Lazima, Asema Migos
Waziri wa Elimu nchini Julius Migos ametangaza kwamba Somo la Hisabati litakuwa la lazima katika shule za upili na kubatilisha tamko la awali la serikali la kulifanya somo hilo liwe la hiari.
Akizungumza wakati wa mtakano wa kitaifa kuhusu uboreshaji wa mtaala wa elimu nchini CBC, Waziri Migos amesema uamuzi huo ulifanywa baada ya wadau mbalimbali kujadili masuala ya CBC kutaka somo la Hisabati kuwa la lazima katika shule za upili.
Waziri Migos amesema wanafunzi ambao watachagua fani ya STEM ikiwemo ni somo la Sayansi, Teknlojia, Uhandisi na Hisabati watasomo Hisabati ya hali ya juu na wanafunzi watakaochagua njia nyingine mbili watasomo Hisabati iliyorahisishwa.
Katika mfumo huo mpya, wanafunzi watachukua masomo manne ya lazima, ambayo ni Lugha ya Ishara ya Kiingereza, Kiswahili, Elimu ya Kimwili, mafunzo ya huduma za jamii na masomo mengine matatu kutoka kwa kundi la chaguzi 38.
Uamuzi huo umejiri baada ya kupata pingamizi hapo awali kutoka kwa Chama cha walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri nchini KUPPET wakiongozwa na Katibu wao mkuu Moses Nthurima kuhusu kulifanya somo la Hisabati kuwa la hiari