Sports

Seville Amshinda Lyles Lausanne, Wanyonyi Apata Pigo Katika Diamond League

Published

on

Mjamaica Oblique Seville alimshinda bingwa wa Olimpiki Noah Lyles katika mbio za mita 100 kwenye mashindano ya Diamond League yaliyofanyika Lausanne jana usiku, ikiwa ni wiki tatu tu kabla ya mashindano ya dunia jijini Tokyo.

Mara nyingine tena, Lyles alichelewa kutoka kwenye vibao vya mwanzo, hali iliyompa Seville nafasi ya kuongoza mapema—aambayo Mjamaica huyo hakuwahi kuipoteza.

Seville alimaliza kwa muda wa kuvutia wa sekunde 9.87 chini ya mvua kubwa katika Stade Olympique de la Pontaise, huku Lyles akijaribu kujitahidi kurejea kwa mwendo wa kasi na kushika nafasi ya pili kwa sekunde 10.02. Hii ilikuwa marudio ya mashindano ya London Diamond League mwezi uliopita ambapo Seville mwenye umri wa miaka 24 pia alimshinda Mmarekani huyo.

“Nimemshinda bingwa wa Olimpiki mara mbili, London na hapa, na hilo linanipa imani kubwa kuelekea mashindano makuu. Imekuwa muda mrefu tangu Mjamaica kushinda mita 100 kwenye mashindano ya dunia, na bila shaka naamini mimi ndiye nitaifanya,” alisema Seville.

Lyles, kwa upande wake, alijilaumu akisema alihisi “mwitikio mbaya sana kwenye bastola ya kuanzia. Hilo ndilo kosa pekee.”

“Kiufundi nilihisi niko vizuri, mazoezi ya kujiandaa yalikuwa mazuri, lakini ukichelewa kuanza kwenye kiwango hiki, basi mbio huwa zimeisha,” aliongeza.

“Kimwili nahisi niko vizuri, na nina imani kila mbio zitanipa mwendelezo bora zaidi. Lengo ni kuboresha maelezo madogo hasa mwendo wa mwanzo na kasi yangu ya kwanza kuelekea Tokyo na mashindano ya dunia.”

  • Hoey aongoza –

Bingwa wa Olimpiki kutoka Kenya kwenye mita 800 Emmanuel Wanyonyi pia alipata pigo baada ya Mmarekani Josh Hoey kushinda mbio hizo.

Hoey, bingwa wa dunia wa ndani ya ukumbi (indoor), alijihakikishia ushindi katika mita za mwisho na kumaliza kwa muda wa dakika 1:42.82.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version