Business
Serikali Yatenga Bilioni 4.5 Kuimarisha Vyama vya Ushirika na Kilimo
Serikali kuu imetenga shilingi bilioni 4.5 kusaidia vyama vya ushirika, akiba na mikopo ili kuimarisha kilimo humu nchini.
Akizungumza na vyombo vya habari mkuu wa mawaziri nchini Msalia Mdavadi amevitaka vyama vya ushirika kutumia mfumo wa kidigitali ili kuimarisha mapato yao.
Mdavadi amepongeza vyama vya ushirika akisema vimechangia kuimarika kwa uchumi wa taifa.
Aidha mdavadi amesema serikali imejitolea kurejesha pesa zilizotumiwa visivyo kwenye vyama vya ushirika, muungano wa vyama vya akiba na mikopo kusco na itawachukulia hatua za kisheria wahusika.