News
Serikali Kubuni Sera Itakayotambua na Kuthamini Wadhfa wa Wazee wa Mitaa
Serikali imeanzisha mpango wa kubuni sera itakayotambua na kuthamini wadhfa wa wazee wa mitaa na wale wa nyumba kumi ili kuimarisha usalama hadi mashinani.
Katika makadirio ya sera ya kitaifa ya utawala ya vijijini, mpango huo ni muhimu kwani unalenga kuidhinisha wadhfa wa Wazee wa mitaa katika muundo wa utawala wa taifa.
Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen amesema serikali inalenga kutekeleza sera hiyo ili kuleta ujumuishi wa utawala wa mikao kwani maeneo mengi nchini yamekuwa wakikabiliwa na changamoto za kiusalama.
Waziri Murkomen amewataka wananch kutoa maoni yao kuhusu sera hiyo kabla ya mchakato huo kuzinduliwa rasmi mnamo Aprili 15 mwaka huu katika ofisi zote za utawala wa mikao.
Wakati huo huo, Waziri huyo wa usalama amesema sera hiyo inalenga pia kuwajumuisha wazee wa vijiji katika mifumo ya utawala wa serikali ya kitaifa, akisema hatua hiyo itaongeza urejesho wa kihistoria wa utawala wa kiheshima.