Sports
Serani Waahidi Kutetea Ubingwa Mashindano Ya Shule ya Upili
Mabingwa watetezi wa soka kwa shule za upili kaunti ya Mombasa upande wa wavulana, shule ya upili ya SERANI walianza vyema kampeni ya kutetea taji lao kwa kupata ushindi katika mechi zao zote za makundi.
Katika mechi ya kwanza waliicharaza shule ya upili ya Kajembe 3-0 na Kisha wakawageukia vijana wa shule ya upili ya Khadija na kuwalaza mabao 2-0.Katika mechi zingine, St Charles Lwanga wameona moto kwa kutandikwa 1-0 na Tononoka, Kisha Khadija wakavuna ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Shikaadabu, Moi Forces Academy wakiwachapa St Charles Lwanga 2-0 na Kajembe wakatoka 1-2 dhidi ya Shikaadabu.
Shule ya upili ya Mwakirunge bahati haikuwa upande wao kwani baada ya kupokea kichapo cha mabao 5-0 kutoka kwa Moi Forces katika mechi ya kwanza, hawakuweza kurejea uwanjani kwa kipindi cha pili cha mechi yao ya pili dhidi ya Tononoka ambapo tayari walikuwa wamechapwa magoli 3-0 katika kipindi cha kwanza, wakieleza kuwa hatua hiyo imetokana na wachezaji wengi kupata majeraha wakiwa uwanjani na kubaki na wachezaji 6 pekee.
MOMBASA COUNTY KSSSA DAY 2 FIXTURES