News

Polisi wamjeruhi mchuuzi kwenye maandamano Nairobi

Published

on

Maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia siku ya Jumanne 17, Juni 2025 walimfyatulia risasi mchuuzi mmoja aliyekuwa akiuza barakoa karibu na barabara ya Moi katikati mwa jiji la Nairobi wakati wa maandamano ya vijana wa Gen Z, yakutaka Naibu Inspekta jenerali wa polisi Eliud Lagat ajiuzulu.

Katika video iliyosambaa  kwenye mitandao ya kijamii, maafisa wawili wa polisi walionekana wakimkandamiza mchuuzi kando ya barabara ya Moi jiji humo na kuanza kumshushia kipigo.

Mmoja wa maafisa hao alishika bunduki na kumpiga risasi mtu huyo kwa karibu kabla ya kuondoka eneo la tukio.

Kufuatia tukio hilo, wasamaria wema kadhaa walionekana wakiwa wamembeba mtu huyo ili kunusuru maisha yake.

Video hiyo tangu wakati huo imeibua hisia miongoni mwa wakenya huku wakitaka haki itendeke dhidi ya ukatili wa polisi.

Rais wa Chama cha mawakili nchini LSK Faith Odhiambo, pia aliitaja hali hiyo kama isiyokubalika.

Waandamanaji katika miji mbali mbali nchini waliendelea na maandamano ikiwemo jijini Mombasa na mjini Kilifi, wakimshinikiza naibu inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat kujiuzuli kabisa, baada ya kutangaza kujiuzulu kwa mda siku ya jumatatu juni 16 wakati alipohusishwa na mauaji ya mwanablogu Albert Ojwang’.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version