News
Polisi wa Kenya afariki nchini Haiti
Huduma ya kitaifa ya polisi nchini NPS imethibitisha kufariki kwa maafisa mmoja wa polisi anayehudumu katika kitengo cha kudhibiti amani na usalama nchini Haiti MSS.
Katika taarifa iliyotolewa na idara ya Polisi nchini na kutiwa saini na Msemaji wa idara ya Polisi nchini Michael Nyaga Muchiri, ilisema afisa huyo wa Polisi alipoteza maisha yake baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani.
Michiri alisema ajali hiyo iliyokea katika barabara ya Kenscoff-Petion-Ville katika eneo la Pelerin 9 wakati wa oparesheni ya uokoaji inayohusisha magari mawili ya Maxxpro.
Ajali hiyo pia ilisababisha maafisa wengine wanane wa kitengo hicho cha MSS kujeruhiwa huku watatu kati yao wakiwa katika hali mbaya zaidi hospitalini nchini Haiti huku ikisema mikakati na mipango ya kusafirisha mwili wa afya huyo hadi nchini Kenya inaendelea.
Taarifa hiyo hata hivyo ilisema itahakikisha maafisa wa polisi wa Kenya kwa ushirikiano wa maafisa wa polisi wa taifa la Haiti wanapambana ili kuhakikisha amani na usalama unashuhudiwa nchini humo.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi