National News
Omollo Awarai Vijana Kudhibiti Uhalifu wa Mitandao
Katibu katika Wizara ya usalama wa ndani nchini Dkt Raymond Omollo amewarai wanasiasa na wafanyibiashara nchini kuisaidia serikali kufanikisha ajenda yake ya miradi ya maendeleo mashinani.
Omollo amesema hatua hiyo itahakikisha wananchi mashinani wananufaika moja kwa moja na mipango ya serikali ya maendeleo, akisisitiza haja ya wanasiasa kuwa mstari wa mbele kueleza sera za serikali kwa wananchi.
Omollo, hata hivyo amewarai vijana walio na ufahamu zaidi katika maswala ya utandawazi kuhakikisha wanadhibiti uhalifu wa mtandao, akisema umechangia taifa kushuhudia uovu mwingi.
Wakati huo huo ameahidi kwamba serikali kupitia Wizara ya usalama nchini itahakikisha wananchi wako na usalama wa kutosha, akisema juhudi hizo pia zitafaulu kupitia ushirikiano.