News

Odinga, awasuta wapinzani dhidi ya kauli ya Wantam

Published

on

Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga ameonekana kuunga mkono ushirikiano kati ya chama cha UDA na ODM, na akawasuta wapinzani dhidi ya kauli yao ya Wantam.

Odinga aliwataka wakenya na upinzani kuipa nafasi serikali kukamilisha ajenda yake na kisha wananchi watafanya uamuzi wao ifikapo uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027. 

Akizungumza wakati wa mazishi ya Pheobe Asiyo katika kaunti ya Homabay, Odinga aliweka wazi kwamba juma lijalo kutakuwa na mkutano wa Muungano wa wabunge ambao utaangazia masuala mbalimbali muhimu. 

“Niko na imani kwamba masuala mbalimbali anayoihusu taifa yatatekelezwa na tunaomba mtupe nafasi kisha ikifika uchaguzi mkuu mwaka 2027 wakenya ndio wataambua sio tu kubweka bweka na Wantam wantam”, alisema Odinga.

Wakati huo huo aliitaka serikali kufanikisha mchakato wa fidia kwa wananchi ambao wamepoteza maisha yao wakati wa maandamano ya ghasia, akisisitiza suala kangazia majanga ya maandamano ya mwaka wa 2017. 

Kauli za viongozi hao zimejiri baada ya kuafikiwa mpango wa kufanikisha ajenda 10 kwenye mkataba wa ushirikiano wa kitaifa kati ya chama cha UDA na ODM pamoja na kuidhinishwa kwa ripoti ya NADCO.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version