News

Odinga, anataka fedha za NG-CDF kusambazwa kwa kaunti

Published

on

Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga amependekeza fedha zote zinazosambaza kwa hazina ya NG-CDF na NGAAF, kufanywe marekebisho ili fedha hizo kusambazwa kwa serikali za kaunti.

Odinga alisema kila kitu ambacho wakenya wamefanya ni kurudisha utawala bora, na wamefanya hazina ya NG-CDF kuwa ya kizamani na kwamba fedha hizo zinafaa kutumwa kwa serikali za kaunti kwani hazina hiyo hatambuliki kikatiba.

Akihutubia Kongamano la Ugatuzi katika kaunti ya Homabay, Odinga alishikilia msimamo wake kwamba ni lazima ugatuzi upewe kipau mbele na masuala yote yaliyogatuliwa kusimamiwa na serikali za kaunti. 

“Hazina ya NG-CDF na NGAAF zinapokea fedha nyingi na kutumika kwa mambo ya basari, hii pesa inafaa kutumwa kwa serikali za ugatuzi kwani hazina ya NG-CDF ilipitwa na wakati na hatambuliki kikatiba na iwapo kutafunywa marekebisho basi pesa hizo zitasaidia ugatuzi kuimarika zaidi”, alisema Odinga.

Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga katika Kongamano la ugatuzi, Homabay{Picha kwa hisani}

Wakati huo huo amevisuta vyombo vya habari, akisema baadhi ya vyombo vya habari nchini vimekuwa vikilipwa ili kufichua sakata za ufisadi nchini, akisema ni lazima kila mmoja achukue jukumu la kupambana na ufisadi.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version