Mahakamani ya Shanzu imeagiza kuzuiliwa kwa siku 14 kwa mshukiwa wa mauaji ya mtoto Keziah Matuki, aliyekuwa na umri wa miaka 7.
Mahakama imetoa agizo hilo baada ya maafisa wa idara ya upelelezi wa jinai DCI kuiomba Mahakama kuwapa muda zaidi wa kukamilisha uchunguzi wao na kuwasilisha ushahidi Mahakamani.
Maafisa hao wamesema wanataka muda zaidi ili kukamilisha uchunguzi wao, ambapo mshukiwa atafanyiwa vipimo vya DNA katika maabara ya serikali, kuhojiwa zaidi kuhusu tukio hilo, pamoja kuwasilishwa kwa ripoti ya madaktari ya upasuaji wa miati Mahakamani.
Mshukiwa huyo kwa jina Dennis Otieno Oduor kwa jina maarufu Dennis Mkikuu Mwobolo, anadaiwa kutekeleza kitendo hicho cha kinyama kwa mtoto huyo ikiwa ni pamoja na kumnajisi na kumnyonga na kisha kumvunja shingo.

Mshukiwa wa mauaji ya mtoto Keziah, Dennis Otieno Oduor kwa jina maarufu Dennis Mkikuu Mwobolo, afikishwa katika Mahakama ya Shanzu
Tukio hilo linadaiwa kutekelezwa mnamo tarehe 3 mwezi Mei mwaka huu katika kijiji cha Kwa Nzai eneo la Mwezang’ombe kaunti ya Kilifi.
Kesi hiyo itatajwa tena mnamo tarehe 25 mwezi Mei mwaka huu.
