Maafisa wa Polisi katika kituo cha Mtwapa katika kaunti ya Kilifi wamefanikiwa kumkamata mshukiwa mmoja wa wizi na kunasa mali mbalimbali zinazoshukiwa kuibwa.
Kukamatwa kwa mshukiwa huyo kumetoka na oparesheni maalum ya kijasusi iliyotekelezwa ndani ya mji wa Mtwapa.
Kupitia taarifa ya maafisa wa Polisi, maafisa hao wamesema walifaulu kupata bidhaa kadhaa zikiwemo mitungi ya gesi, simu za mkononi, runinga, vifaa vya kielektroniki, vifaa vya matumizi ya nyumbani, laini za simu pamoja na vifaa vingine.

Maafisa wa polisi eneo la Mtwapa wamefaulu kunasa bidhaa mbalimbali zilizoibiwa katika mji wa Mtwapa kaunti ya Kilifi.
Mshukiwa huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Mtwapa akisubiri kufikishwa mMahakamani huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
Aidha bidhaa zilizopatikana zimehifadhiwa kama ushahidi utakaotumika katika kesi hiyo Mahakamani.
Maafisa hao hata hivyo wamesema oparesheni ya kuwasaka wahalifu katika mji wa Mtwapa utaendelea ili kuhakikisha visa vya uhalifu vinakomesha na usalama kuimarishwa zaidi katika mji huo na kaunti nzima ya Kilifi.
Taarifa ya Mwanahabari wetu.
