Kenya na Ufaransa zimetia saini mikataba ya bilioni 104

Kenya na Ufaransa zimetia saini mikataba ya bilioni 104

Kenya na Ufaransa zimetia saini makubaliano ya kuanzisha ubia wa usafirishaji na maendeleo ya miundombinu ya bandari inayokadiriwa kuwa takribani shilingi bilioni 104.

Makubaliano mengine yanahusu uzalishaji endelevu wa mafuta ya anga, ushirikiano wa kiuchumi wa majini.

Nchi hizo mbili zilikubali zaidi kukuza mauzo ya majani chai ya Kenya kwa masoko ya Ufaransa na kuimarisha ushirikiano katika huduma za afya, elimu na mafunzo ya kiufundi.

Akizungumza wakati wa kutia saini makubalaiano hayo, rais Wiliam Ruto amesema Kenya inalenga kunufaika na utaalamu wa Ufaransa katika nishati ya Nyuklia huku nchi hiyo ikifuatilia lengo lake la kuzalisha megawati 10,000 za umeme.

Rais Ruto ameongeza kuwa Kenya na Ufaransa zimejadili jinsi ya  kuboresha muunganisho wa anga ili kusaidia biashara, utalii na uwekezaji.

Kwa upande wake rais wa ufaransa Emmanuel Macron amesema nchi yake inasalia na nia ya kupanua uwekezaji na ushirikiano kote barani Afrika na kusaidia mageuzi katika mfumo wa fedha wa kimataifa.

Hata hivyo viongozi wanahudhuria Kongamano la la siku mbili la Afrika ambapo zaidi ya marais 30 kutoka bara la Afrika pamoja na wajumbe elfu tatu kutoka mataifa mbalimbali pia nao wko humu nchini kuhudhuria Kongamano hilo. 

Kongamano hilo linafanyika katika ukimbi wa mikutano wa KICC jijini Nairobi, linalenga kuangazia masuala ya muhimu ya kanda ya Afrika.