Bunge la kitaifa linatarajiwa kujadili hoja ya makadirio ya bajeti ya kitaifa ya mwaka wa 2026/2027 ya shilingi trilioni 4.79.
Kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Kimani Ichung’wah aliwasilisha nakala ya bajeti hiyo bungeni ambayo imeongezeka na shilingi bilioni 65 ambayo ni sawa na asilimia 1.92, ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa 2025/2026.
Katika bajeti hiyo, Mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini KRA, inakadiria kukusanya takribani shilingi trilioni 3.629 ili kupiga jeki bajeti hiyo sawa na kufanikisha matumizi ya serikali na utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.
Katika bajeti hiyo, serikali pia inalenga kukopa kima cha shilingi bilioni 995.7 kwa wawekezaji wa ndani kwa ndani ili kuchangia kufanikisha bajeti hiyo ambayo inaonekana kwamba uko juu zaidi.
Kwenye bajeti hiyo, hazina ya kitiafa inalenga sehemu ya ufadhili wa kibiashara kutoka nje ambao umepangiwa shilingi bilioni 145.6, jambo linaloashiria kurejea katika masoko ya kimataifa.

Bunge la kitaifa la Kenya laendelea na vikao vyake bungeni
Sekta ya barabara na uchukuzi imetengea shilingi bilioni 298.5, Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC ikitengewa shilingi bilioni 25.4, sekta ya elimu ikitengewa shilingi bilioni 668.3, sekta ya usalama ikipangiwa shilingi bilioni 566.8, sekta ya afya ikitengewa shilingi bilioni 170.7 huku sekta ya Kilimo kipokea mgao wa shilingi bilioni 62.9.
Hata hiyo serikali za ugatuzi zimetengewa shilingi bilioni 420 licha ya serikali hizo kudai kwamba mgao huo ni mchache na kupendekeza shilingi bilioni 470, huku sekta ya mgao wa shilingi bilioni 9.6 ukitengwa kama mgao wa fedha za zaida.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi
