Mahakama ya Kilifi imemnyima dhamana mshukiwa wa wizi wa kimabavu Amani Mohamed ili kutoa nafasi kwa maafisa wa upelelezi kukamilisha uchunguzi wao.
Hakimu wa Mahakama hiyo Charles Obulutsa ametoa agizo hilo baada ya upande wa mashtaka unaoongozwa na Winnie Otieno kuiambia Mahakama kwamba kesi hiyo inahitaji ufafanuzi zaidi.
Kufuatia ombi hilo la upande wa mashtaka, Hakimu Obulutsa imeagiza mshukiwa kuzuiliwa rumande hadi tarehe 3 mwezi Juni mwaka huu ambapo kesi hiyo itatajwa Mahakamani.
Upande wa mashtaka umeeleza Mahakama kwamba mshukiwa ana rekodi ya uhalifu wa aina sawa hiyo ambayo iko mbele ya Mahakama na kwamba aliwahi kuhudumia kifungo gerezani baada ya kupatikana na hatia ya makosa kama hayo, ikisemekana kuwa ni tabia yake.
Mahakama pia ilielezwa kwamba Amani akiwa na panga alifanya wizi wa mabavu kwa mlalamishi James Mohammed na kumkata kata kwa mapanga hadi akamjeruhi vibaya.
Kesi hiyo itatajwa tarehe 3 mwezi Juni mwaka huu.
Taarifa ya Teclar Yeri
