Wahisi wajitokeza kumsaidia Magastone kuwa na makaazi mpya

Wahisi wajitokeza kumsaidia Magastone kuwa na makaazi mpya

Katika kijiji cha Roka kumekuwa na pilkapilka za ujenzi wa nyumba ya kisasa ambao umetokea kivutio cha wengi kwani unafuatiliwa sana katika mitandao ya kijamii.

Shughuli za ujenzi wa nyumba ya makazi ya Magastone Baraka zilianza majuma kadhaa yaliyopita na wahisani ambao wamejitolea kumjengea Baraka nyumba nzuri ya kuishi.

Baraka alipata ajali mwaka wa 2020 alipoteleza na kuanguka bafuni alipokuwa akioga, ajali ambayo ilisababisha kuvunjika kwa mkono wake mmoja na baada ya miaka mitatu mkono wake huo ukalazimika kukatwa na kubadilikiwa na hali ya kuwakimu wazazi wake pamoja na mchumba wake.

Mambo yalipomzidia na kukumbwa na hali ngumu ya maisha aliziweka habari zake mitandaoni akiwaomba wahisani kumsaidia.

Wahisani mbalimbali waliitikia wito na kujitokeza kumsaidia akiwemo mgombea wa useneta Kilifi Wakili George Kithi, Presenter Kai na mkewe Diana Yegon, ambao wamefanikisha ujenzi wa nyumba hiyo ili kumuwezesha kufanikisha malengo yake ya kuwa na makaazi mapya.

Ujenzi wa Nyumba ya Magastone Baraka eneo la Roka Chumani kaunti ya Kilifi unaendelea

Wengine waliojitokeza kumsaidia na mafundi waliojitolea kuhakikisha Baraka anakuwa na nyumba huku mchango wa shilingi laki moja kutoka kwa Katibu katika Idara ya vijana na uchumi bunifu Fikirini Jacobs.

Mafundi pamoja na vibarua wanaendelea kukamilisha ujenzi wa nyumba ya vyumba viwili, sebule na jiko huku wasanii zaidi wakiahidi kumnunulia samani.

Huu ni mfano mzuri wa kutekelezwa kwa msemo wa Kiswahili nizike ningali Hai, usisubiri kuja kuweka mauwa kaburini.

Taarifa ya Lolani Kalu