Mzozo kuhusu ujenzi wa barabara eneo la Jaribuni katika kaunti ya Kilifi unanukia tena miezi kadhaa baada ya wakaazi eneo hilo kufanya maandamano kulalamikia hali mbaya ya barabara licha ya wawekezaji kufaidika na raslimali za eneo hilo.
Wakaazi eneo hilo, sasa wanapinga mwingilio wa viongozi wanaotaka kumuondoa Mwanakandarasi anayeendelea na ujenzi wa barabara kutoka Jaribuni hadi Tezo, badala yake ujenzi huo uanzie Tezo hadi Jaribuni.
Wakaazi wa eneo hilo wakiongozwa na Mwakilishi wadi ya Jaribuni Peter Shehe wanatishia kuzuia mkandarasi kuendelea na ujenzi wa barabara hiyo, iwapo atahamishwa.
Kulingana na Mwakilishi wadi huyo eneo la Jaribuni kwa mda mrefu limekuwa likitoa bidhaa muhimu za ujenzi na shehemu ya barabara iliyosalia inafaa kukamilishwa kuanzia eneo hilo vyenginevyo wataandamana na kufunga timbo za wanakandarasi.

Mwakilishi wadi ya Jaribuni Peter Shehe akizungumza na Wanahabari kuhusu kuhamishwa kwa mwanakandari wa ujenzi wa barabara ya Jaribuni hadi Tezo
Wakaazi waliokongamana na Mwakilishi wadi eneo hilo wanadai waligundua Tinga Tinga za kutengeneza barabara zilikuwa zimeshitisha Shughuli zake, hali iliyowalazimu kuingilia kati wakimlaumu mbunge wa eneo hilo la Ganze Kenneth Tungule na mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya.

Wakaazi watishia kumzuia mwanakandarasi kuondolewa eneo hilo iwapo viongozi watasimamisha ujenzi wa barabara ya Jaribuni hadi Tezo
Wakaazi hao wanasema kwa mda mrefu wamelalamikia hali mbaya ya barabara licha ya eneo hilo kuwa na raslimali nyingi, wakisema kwa sasa hawatalaza damu na kuwacha mtui yeyote kuingia miradi ya eneo la Jaribuni.
Awali wakaazi wa Jaribuni waliandamana na kufunga barabara, hali iliyolazimu waziri wa Madini Ali Hassan Joho na Gavana wa Kilifi Gedion Mung’aro kuingilia kati, na kufanyikisha ujenzi wa barabara ya lami ya umbali wa Kilomita nane.
Taarifa ya Joseph Jira
