Polisi wanachunguza tukio la mauaji ya Wanawake wanne Kwale

Polisi wanachunguza tukio la mauaji ya Wanawake wanne Kwale

Maafisa wa polisi katika kaunti ya Kwale wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio la mauaji ya Wanawake wanne, ndani ya vyumba za wageni katika meneo ya Samburu, Taru na Meli-kubwa. 

Kamanda wa Polisi eneo la Samburu Lydia Mumbo alisema ripoti iliyotolewa awali ilionyesha kwamba mshukuwa aliwachukua Wanawake hao kwenye vyumba vya wageni kisha kuwanyonga kabla ya kutoroka. 

Lydia alisema mshukiwa huyo pia anadaiwa baada ya kutekeleza kitendo hicho cha kimya alichukua baadhi ya nguo za waathiriwa na kutoroka nazo ili kuficha ushahidi. 

“Tumeona hali sasa imeanza kubadilika na kuwa hatari kwa usalama wa wananchi kwani awali jamaa huyo ambaye bado anasakwa na maafisa wa polisi alikuwa ana njama fiche na kuwauwa wanawake hao katika sehemu tofauti”, alisema Lydia.

Aidha aliwataka Wanawake wanaojihusisha biashara ya ngono kuwa waangalifu zaidi huku akiwarai wananchi kushirikiana na maafisa wa usalama katika kutoa taarifa zitakazochangia kutiwa nguvuni kwa mshukiwa huyo.

“Tunawarai wananchi kuchukua tahadhari na kuripoti wahalifu kwa maafisa wa polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe mara moja na wananchi pia wawe waangalifu”, aliongeza Kamanda huyo wa Polisi.

Taarifa ya Mwanahabari wetu