Zaidi ya watalii 600 wamewasili katika bandari ya Mombasa

Zaidi ya watalii 600 wamewasili katika bandari ya Mombasa

Zaidi ya watalii 600 wamewasili katika bandari ya Mombasa baada ya meli ya kifahari ya Azamara Onward kutia nanga katika bandari hiyo.

Meli hiyo iliyotokea bandari ya Victoria nchini Ushelisheli imebeba watalii 630 pamoja na wahudumu 389 kutoka mataifa mbalimbali, huku wengi wao wakitarajiwa kutembelea vivutio tofauti vya utalii katika eneo la Pwani.

Meli ya watalii zaidi ya laki sita ya Mv Azamara Onward imetia nanga katika Bandari ya Mombasa

Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Naibu Mwenyekiti wa kamati ya bunge la kitaifa kuhusu masuala ya wakenya wa Ughaibuni na wafanyakazi, Simon King’ara, amepongeza Wizara ya Utalii kwa juhudi za kuitangaza Kenya katika soko la kimataifa.

“Tumepokea watalii zaidi ya laki sita na tunashukuru hii ni ishara wazi kwamba sekta ya utalii inaendelea kuimarika na tayari watalii wengine wanatemebelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii kujinjari na kunapongeza serikali kwa kuhakikisha sekta hii inapigwa jeki vizuri”,alisema King’ara.

Watalii waliowasili nchini Kenya watumbuizwa na wasakata densi wa kitamaduni ya jamii ya Pwani.

Kwa upande wake, Mawakala wa meli hiyo wakiongozwa na Hashim Ahmed walisema kuongezeka kwa safari za watalii nchini Kenya ni ishara kuimarika kwa sekta hiyo pamoja na uchumi wa taifa. 

“Tunaipongeza serikali, Wizara ya utalii na bandari kuhakikisha sekta hii inamarika zaidi na tunawaomba waweka mikakati bora” aliongeza Ahmed.

Meli hiyo itasalia katika bandari ya Mombasa kwa siku mbili kabla ya kuendelea na safari yake nchini Zanzibar.

Taarifa ya Mwanahabari wetu