Mvua ambayo inaendelea kunyesha nchini imesababisha baadhi ya barabara zilizoko mashinani katika wadi ya Sokoni eneo bunge la Kilifi Kaskazini kaunti ya Kilifi kutopitika kwa urahisi.
Hali hii imetokana na ubovu wa barabara hizo ambazo kwa sasa zimefurika maji.
Hali hii pia
imesabisha wanaotumia barabara hizo wakiwemo wahudumu wa pikipiki wa maeneo ya Kiwandani na Kashem kulalamikia madhila ambayo wanayapitia.Walisema imekuwa vigumu hata kwa akina mama wajawazito na wagonjwa wanaotumia barabara hizo kupata huduma za matibabu katika zahanati ya Kiwandani.
Kwa upande wa wafanyabiashara nao walilalamikia kupungua kwa wateja kutokana na maji yanayotuama kwenye maeneo yao ya biashara.
Kwa pamoka walitoa wito kwa mwakilishi wa wadi ya Sokoni Ray Mwaro, mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Bayan na Gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Maitha Mungaro kuingilia kati ili kupatikane suluhu la kudumu.
Taarifa ya Janet Mumbi
