Mahakama ya Kilifi yamuachilia kwa dhamana mshukiwa wa unyakuzi wa ardhi

Mahakama ya Kilifi yamuachilia kwa dhamana mshukiwa wa unyakuzi wa ardhi

Mahakama ya Kilifi imemuachilia kwa dhamana ya shilingi laki tano na mdhamini wa kiasi sawa na hicho George Mweni Muramba anayekabiliwa na shtaka la unyakuzi wsa ardhi.

Mweni anadai kufanya usajili wa shamba mali ya Gulmohamed Khamis Shapi.

Hakimu wa Mahakama hiyo Ivy Wasike ametoa agizo hilo baada ya mshukiwa kukana madai yaliowasilishwa Mahakamani kwamba tarehe 21 mwezi Februri mwaka 2024 katika ofisi za usajili wa ardhi Kilifi kazkazini kaunti ya Kilifi, Mweni alifanya usajili wa ardhi nambari Kilifi/ Madeteni/367 akijua kuwa ardhi hiyo ilikuwa imeuziwa Gulmohamed Khamis Shapi.

Mahakama pia imeelezwa kwamba tarehe tofauti kati ya mwaka 2019 hadi 2022, Mweni alifanya ulaghai wa pesa shilingi milioni moja nukta nne [1,460,000] mali Andrew Kithi Kombe akisema kuwa angemuuzia ekari nusu ya ardhi hiyo ambayo haikuwa yake.

Vile vile mnamo tarehe tofauti ya mwezi Machi mwaka 2024, Mweni alimlaghai Judithi Adawo Otieno shilingi milioni nne nukta nne [4,400,000] akisema kuwa angemuuzia ekari 2.2 sehemu ya ardhi hiyo.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe 23 mwezi Septemba mwaka huu wa 2026.

Taarifa ya Teclar Yeri