Uchunguzi wa ajali ya ndege iliyosababisha kifo cha Ng’eno umeanza

Uchunguzi wa ajali ya ndege iliyosababisha kifo cha Ng’eno umeanza

Uchunguzi wa ajali ya ndege aina ya Helkopta iliyowaua watu sita akiwemo Mbunge wa Emurua Dikirr Johana Ng’eno umeanza rasmi huku wachunguzi wakifika katika eneo la tukio.

Wataalam na wachunguzi wa ajali za ndege wamekusanya vifaa na mabaki ya ndege kutoka eneo Chepkiep kwenye msitu wa Mosop Kaunti ya Nandi ambapo ajali hiyo ilitokea.

Maafisa hao wako makini kubaini chanzo cha ajali hiyo iliyowauawa watu hao huku Kaimu mkurugenzi wa idara ya uchunguzi wa ajali za ndege Fredrick Kabunge akisema sehemu muhimu tayari zimehifadhiwa na zitasaidia kubaini kilichosababisha ndege hiyo ya kampuni ya Youth Aviation kuanguka.

Naye Katibu katika Wizara ya uchukuzi Teresiah Mbaika alitaka uchunguzi kufanywa mara moja na ripoti hiyo kutolewa huku akitoa wito kwa wananchi na viongozi kuwa na subira.

Kwa upande wake Katibu katika Wizara ya usalama nchini Raymond Omollo alisema uchunguzi wa kwanza umebaini kuwa hali mbaya ya anga kutokana na mvua nyingi inayonyesha kuwa iliachangia kwa ajali na kuwataka Wakenya kusubiri uchunguzi kamili.

Taarfa ya Janet Mumbi