Mwadime awaonya wakenya wanaosaka ajira ughaibuni

Mwadime awaonya wakenya wanaosaka ajira ughaibuni

Serikali imetahadharisha wakenya kuwa makini hasa wanapoahidiwa ajira katika mataifa ya ughaibuni ili kuepuka kulaghaiwa au kujikuta katika hali hatarishi.

Katibu katika Wizara ya Leba nchini Shadrack Mwadime, alisema inasikitisha kuona takriban wakenya elfu moja wanatumika kupigania vita vya Ukraine naUrusi wakiweka maisha yao hatarini.

Mwandime alisema hali hiyo imepelekea baadhi ya wakenya wanaoshiriki mapigano hayo kupoteza maisha.

“Ni lazima wakenya wanaosaka ajira katika mataifa ya ughaibuni kuwa makini na mawakala wanaodai kuwatafutia ajira kwani wengi wao wamekuwa wakihadaiwa”, alisema Mwadine

Aidha amoengeza kwamba wakenya hao walitumia njia za mkato kusafiri katika mataifa hayo akibainisha kwamba mikakati ya serikali ya kuabiliana na hali hiyo inaendelea.

Taarifa ya Joseph Jira