Matiangi: Hautaiba kura zetu

Matiangi: Hautaiba kura zetu

Naibu Kinara wa Chama cha Jubilee Dkt Fred Matiangi ameitaka serikali kuwajibika kikamilifu kwa kuhakikisha taifa linazingatia usalama wa wananchi.

Matiangi alisema jinsi hali ilivyo kwa sasa nchini ni wazi kwamba serikali imeshindwa kutekeleza majukumu yake pamoja na kutosikiza maoni ya umma na huenda hali hiyo ikatatiza taifa lenye kuzingatia amani na demokrasia.

Akizungumza baada ya kuhudhuria ibada ya Jumapili, Matiangi aliitaka serikali kusikiza ushauri wa viongozi wa kidini mwenye malengo ya kuiwezesha serikali kuwatumikia wananchi.

“Serikali imeshindwa kusikiza maoni ya umma na inachangia taifa lenye amani kurudi katika vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa maandamano ya vijana wa Gen Z mwezi Juni mwaka 2024”, alisema Matiangi.

Akigusia suala la uchaguzi mkuu ujao, Matiangi amewaonya wenye malengo ya uwizi wa kura.

” Wewe wewe hutaiba kura zetu tena”, aliongeza Matiangi.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi