Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen amewaonya wakenya wanaoendeleza siasa za vurugu, fujo na ukabili, akisema watu hao wataandamwa na mkono wa sheria.
Waziri Murkomen aliwataka wanasiasa kufanya kampeni zao kwa usawa na haki na wala sio kuzikejeli jamii zengine nchini, akisema serikali kupitia idara ya usalama haitakubali uchochezi wa kikabili nchini.
Aidha aliweka wazi kwamba kama Waziri wa usalama wa ndani atahakikisha wakenya wote wanapata huduma sawa za kiusalama huku akiwaonya wanasiasa dhidi ya tabia ya kumdhalilisha Inspekta jenerali wa polisi nchini Douglas Kanja.
Waziri huyo wa usalama wa ndani amehoji kwamba siasa za ukabili, matusi na majivuno haitasaidia taifa lililojikita katika masuala ya demokrasia kupiga hatua kimaendeleo, akisisitiza haja ya kila mmoja kupewa heshima.
“Wewe uza sera zao sio eti kabili hii kabila hii yani ni kama ambaye hakuna kabila zengine humu nchini apana hiyo hatutakubali na muache kudharua Inspekta jenerali wa polisi, tutawakujua kwa sababu hatutakubali hiyo maneno”, alisema Murkomen.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi
