NIS: Wakenya elfu moja wako kwenye vita kati ya Urusi na Ukraine

NIS: Wakenya elfu moja wako kwenye vita kati ya Urusi na Ukraine

Idara ya ujasusi nchini NIS imetoa ripoti yake kuhusu suala la usalama na kuweka wazi kwamba zaidi ya wakenya elfu moja wanashiriki katika vita kwenye mataifa ya ulaya kati ya Urusi na Ukraine.

Ripoti hiyo ilisema usajili wa wakenya kupigana nchini Urusi uimechangiwa na maafisa wa serikali wakiwemo maafisa wa uhamiaji, maafisa wa idara ya upelelezi wa jinai DCI na wale wa mamlaka ya kitaifa ya uajiri.

Akisoma ripoti hiyo wakati wa vikao vya bunge siku ya Jumatano Februari 19, 2026, Kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Kimani Ichung’wah, alisema kampuni mmoja ilitumika kuwasajili baadhi ya wakenya kujiunga na vita hivyo bila kujua kwani wengi walikuwa na fikra za kufanya kazi ya udereva.

Ichung’wah alifafanua kwamba katika usajali huo kuna hospitali mbili zilitumika na ukaguzi wa kiafya kwa wale waliosajiliwa kujiunga na vita hivyo bila ya ufahamu wowote kwani kiwanja cha ndege ya kimataifa ya JKIA ilitumika.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi