Serikali imesema imelipa bili zote ambazo hazikuwa zimelipwa kwa Wanakandarasi wa barabara, ambazo zimefikia shilingi bilioni 177 za miradi ya tangu mwaka wa 2020.
Naibu Rais Kithure Kindiki amesema ulipaji wa bili hizo, utawezesha kuanza tena kwa ujenzi wa barabara ambao zilikuwa zimesimama kwa miaka kadhaa kutokana na kutolipwa kwa wanakandarasi hao.
Kindiki ameyazungumza hayo baada ya kupokea ripoti ya miradi ya maendeleo ikiwemo barabara, madaraja na miundombinu mingine ambayo inatekelezwa na Wizara ya barabara na uchukuzi nchini.
Aidha amesema serikali inafanya kila juhudi kuhakikisha inapata fedha za kukamilisha kilomita elfu 6 za barabara ili kuepusha ucheleweshaji wa malipo kwa Wanakandarasi waliopewa zabuni za ujenzi wa barabara nchini.
Wakati huo huo ameitaka Wizara hiyo ya barabara na uchukuzi nchini pamoja na Wanakandarasi kuzingatia viwango vya juu zaidi vya ubora na kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi
